Tuesday, 10 May 2016

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya May 10,

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema uhaba wa sukari uliopo kwa sasa nchini umesababishwa na Rais

Akihojiwa na Mtangazaji Yvonne Kamuntu kwenye Azam News, Mchumi mbobezi hapa nchini Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema uhaba wa sukari uliopo kwa sasa nchini umesababishwa na Rais John Magufuli mwenyewe kwa kuzuia sukari ya nje kutoingizwa Nchini, ilhali viwanda vyetu havikidhi idadi inayohitajika katika uzalishaji wake.

Pia Prof. Lipumba amesema hakuna sheria inayoruhusu Serikali au Bodi ya Sukari kupanga bei ya sukari nchini hivyo ametaka siasa kuacha kutumika katika mambo serious na wafanyabiasahara wasitishwe.

Swala la Sukari lisitu sahaulishe Lugumi na Ripoti ya CAG..... tusiwe wepesi wakutolewa kwenye Reli, Lugumi na Ripoti ya CAG imeishia wapi ama inaendeleaje?

Hivi ile kamati ya PAC imeishia wapi na ishu ya Lugumi? Mbona hapa pako kimya? Na tukizingatia ni ishu inayogusa jeshi letu la polisi? Hapa jipu halitumbuliki?

Nimejiuliza maswali hayo nikasema nilini Watanzania tutalazimisha Watawala wajue tumechoka na kusikia ishu zikiibuliwa na kuishia njia.... Au huko Bungeni wanaliongelea na sisi huku hatusikii wala kuona kwakuwa Bunge halipo live?

Swala la Sukari lisitu sahaulishe Lugumi na Ripoti ya CAG..... tusiwe wepesi wakutolewa kwenye Reli, Lugumi na Ripoti ya CAG imeishia wapi ama inaendeleaje?

HUU MCHEZO HAUHITAJI HASIRA

By Henry Kilewo

Wizkid azidi kung’ara duniani BILLBOARD HOT 100 TOP 10 awa no1 kwa Drake feat. Kyla & WizKid – “One Dance”

Jina la Wizkid linazidi kung’ara duniani, shukrani kwa shavu alilopewa na Drake.

Wimbo ‘One Dance’ wa Drake aliomshirikisha msanii huyo wa Nigeria umekamata nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100. Wimbo huo upo kwenye album ya Drake, Views ambayo pia nayo imeshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard 200 chart.

BILLBOARD HOT 100 TOP 10

1. Drake feat. Kyla & WizKid – “One Dance”
2. Desiigner – “Panda”
3. Lukas Graham – “7 Years”
4. Mike Posner – “I Took a Pill in Ibiza”
5. Fifth Harmony feat. Ty Dolla $ign – “Work from Home”
6. Rihanna feat. Drake – “Work”
7. The Chainsmokers feat. Daya – “Don’t Let Me Down”
8. Zayn – “Pillowtalk”
9. Calvin Harris feat. Rihanna – “This is What You Came For”
10. Justin Bieber – “Love Yourself”
Wakati mchungaji wa Kanisa la Moravian akikamatwa na meno ya tembo 11 ndani ya kanisa, huko Moshi wachungaji wawili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji. Tukio la wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro linawahusisha wachungaji wawili wa KKKT, Rodrick Mlay (52) na Godbess Mamkwe (38) pamoja na wananchi watatu ambao jana walipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini humo kwa madai ya kuua kwa kukusudia. Wakati wachungaji hao wawili wakipanda kizimbani, Polisi mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wanawashikilia watu wawili akiwamo mchungaji wa Kanisa la Moravian kwa tuhuma ya kunaswa wakiwa na meno ya tembo 11 wakiwa wameyahifadhi ndani ya kanisa. Akizungumzia meno hayo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi katika Kanisa la Moravian lililopo Kijiji cha Usevya, Wilaya ya Mlele. Nyanda alisema mchungaji huyo akiwa na mwenzake ambao wote majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za upelelezi, walikamatwa kufuatia taarifa zilizolifikia jeshi hilo na askari wa hifadhi kuwa, watu hao wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na wamekuwa wakiyahifadhi ndani ya kanisa. Baada ya taarifa hizo, polisi na askari hao walifanya uchunguzi kuhusiana na taarifa hizo kwa kufika katika kanisa hilo na kufanya upekuzi uliofanikisha kukamatwa kwa meno hayo yakiwa yamehifadhiwa kwenye tenga la kubebea mizigo. Kaimu kamanda huyo alisema katika matukio mengine mawili tofauti yaliyotokea Mei 8, saa mbili usiku kwenye maeneo ya Mgolokani, Kata ya Sitarike wilayani humo, polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi hiyo walimkamata mtu mmoja akiwa na jino moja la tembo. Nyanda alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya askari kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake na kukamata jino hilo na lingine la simba. Alisema wote waliokamatwa kwenye matukio hayo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma zinazowakabili. Katika tukio la wachungaji waliofikishwa mahakamani mjini Moshi, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Julieth Mawole alisema wakiwa na wananchi watatu aliowataja kwa majina ya Fadhili Mkenda (36), Jackson Ruben (45) na Mathayo Moses (27), Mei 4 katika eneo la Kilema Pofo wanadaiwa kumuua kwa makusudi Frank Peter (19). Hakimu Mawole aliwataka watuhumiwa hao kutojibu lolote na kesi dhidi yao itasikilizwa Mei 23 katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi na wote walipelekwa rumande kwa sababu shtaka waliloshtakiwa nalo halina dhamana kisheria. Katika hatua nyingine, raia wa Marekani, Mbaraka Mtambo (50) amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na maganda mawili ya kobe bahari aliyokuwa ameyafichwa kwenye begi la nguo. Kamanda wa Polisi wa JNIA, Martin Otieno alisema raia huyo mwenye asili ya Tanzania, alikamatwa juzi saa 3.45 usiku akijiandaa kwa ajili ya safari ya kwenda Marekani na ndege ya Shirika la KLM kupitia Uholanzi.

Monday, 9 May 2016

sukari tani 133 za sukari iliyoingizwa kimagendo yagawiwa bure


Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.

Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.

Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Milioni 246.

Sukari hiyo imegawiwa kwa taasisi 31 mkoani humo baada ya TFDA kuthibitisha kuwa sukari iko salama kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo TRA kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, iliamriwa sukari hiyo kuigawa kwa watu wenye uhitaji katika mkoa huo zikiwemo taasisi za elimu, Afya, kambi za wazee na Jeshi la magereza.

Chanzo: TBC

rais magufuli awagomea wabunge nyongeza ya mikopo ya magari


Katika kile kinachoonekana amedhamiria kuendelea kubana matumizi ya serikali, Rais John Magufuli amekataa ombi la kuongeza fedha za ununuzi wa magari kwa wabunge pamoja na fedha za mfuko wa bunge.

Baada ya kuchaguliwa, wabunge walipatiwa milioni 90  za mkopo kwa ajili ya ununuzi wa magari, lakini baadhi yao walieleza kutoridhishwa na kiasi hicho, wakidai hakitoshelezi na kutaka kiongezwe hadi sh. milioni 120.

Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa wabunge waliwasilisha ombi kwa Rais Magufuli kuongezwa fedha lakini ombi hilo limekataliwa.

Chanzo cha kuamini kimedokeza kuwa mmoja wa wabunge wa CCM alimkumbushia Rais Magufuli ombi hilo wakati wa kikao cha chakula cha jioni, kilichofanyika wiki iliyopita mjini Dodoma.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli alikataa kuwaongezea wabunge fungu hilo kwa madai kuwa serikali yake haina fedha.

Kilieleza pia kuwa Rais Magufuli alikataa kuongeza fungu la mfuko wa jimbo kwa kuwa serikali haina fedha huku akiwataka wabunge kufanya kazi kwa bidii.

"Rais alisema kwa sasa hali si nzuri, amekumbana na changamoto mbalimbali na kutuahidi kulichukua ombi letu, endapo hali itatengemaa atatuangalia kwa sababu hata yeye analitambua hilo kwa sababu alikuwa mbunge."Kilisema chanzo hicho

floyd mayweather kurudi tena ulingoni


FLOYD MAYWEATHER na staa wa UFC, Conor McGregor wapo mbioni kuingia ulingoni kuzichapa kwenye pambano kubwa na aghali zaidi la masumbwi katika historia.

Gazeti la The Sun limedai kuwa Mayweather, anatarajia kuzichapa na staa huyo jijini Las Vegas mwaka huu.

Mayweather alitangaza kustaafu ndondi akiwa ameshinda mapambano yote 49 aliyowahi kupigana. Kwenye pambano hilo Mayweather atachukua paundi milioni 100 huku McGregor atachukua paundi milioni 7.

Tangazo rasmi litatolewa wiki chache zijazo.

Chanzo kililiambia gazeti la The Sun kuwa Floyd alichukia baada ya Conor kudai anaweza kumtwanga KO ndani ya sekunde 30 tu na sasa anataka kumuonesha kazi.

soma habari zilizopo katika magazeti yaleo tarehe 9



SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya May 9, Ikiwemo ya Sukari iliyofichwa yagawiwa Bure